• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Tunduma TC Kuinua Uchumi wa Wanawake

Imewekwa : December 28th, 2023

Na Julius Evandino na Hajra Hashim, Tunduma TC

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Belton Garigo, amewahakikishia Wanawake kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kuwaunga mkono katika shughuli za kiuchumi wanazozifanya ili kuchochea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Garigo ameyasema hayo leo tarehe 28 Disemba 2023 wakati akifungua Kongamano la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi lililofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tunduma TC, Tunduma mjini.

Kiongozi huyo amewataka wanawake kuwa na maandalizi ya kutosha na mipango endelevu ya kukuza na kuendeleza fedha walizonazo na wanazotarajia kukopeshwa na Serikali  kupitia mikopo ya asilimia kumi ambayo itaanza kutolewa mara tu Serikali itakapotoa muongozo na utaratibu wa ukopeshaji baada ya kuisitisha kwa muda.

Aidha, Garigo amewasihi washiriki wa Kongamano hilo kuendelea kutoa elimu kwa Wanawake wenzao dhidi ya vitendo vya ukatili kwa jamii hasa watoto.

“Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia ukatili unaofanywa na wanawake wenzenu ikiwemo kutupa watoto na wengine kutelekeza familia zao.” Amesema Garigo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji  Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Songwe, Zilpa Simchimba amewataka Wanawake kudumisha mila na desturi  kwa kuwa na heshima kwa wenza wao na kujishusha ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima inayofanya familia zisambaratike na kusababisha watoto waishio mitaani na katika Mazingira magumu na hatarishi.

Uanzishwaji wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi nchini yalizinduliwa  rasmi tarehe 06 Juni 2016 na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo ambaye kwa sasa ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuwakutanisha Wanawake katika ngazi zote za jamii ili kujadili fursa na changamoto zinazowakabili katika shughuli za kiuchumi.

Matukio katika Picha:

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Belton Garigo akizungumza wakati akifungua Kongamano la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi la Halmashauri hiyo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 28 Disemba 2023.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Songwe, Zilpa Simchimba akizungumza wakati wa Kongamano la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi la Halmashauri ya Mji Tunduma lililofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 28 Disemba 2023.

Mratibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Halmashauri ya Mji Tunduma, Edward Mbembela akizungumza wakati wa Kongamano la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi la Halmashauri hiyo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 28 Disemba 2023.

Matukio katika picha wakati wa Kongamano la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi la Halmashauri ya Mji Tunduma lililofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 28 Disemba 2023.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa