• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

PJT MMMAM Yazinduliwa Rasmi Tunduma

Imewekwa : February 9th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi amezindua rasmi Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), hafla ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kihongosi amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali zinazomgusa mtoto, imeandaa Programu hiyo ya miaka mitano (2021/2022 - 2025/2026) ili kuwalinda watoto na kuwaimarisha katika malezi na makuzi yao ili kuwa na taifa imara kwa siku zijazo.

“Niwaombe sana Wazazi tujitahidi kuwalinda na kuwatunza ipasavyo watoto wetu…kiukweli watoto kwa sasa wapo katika changamoto kubwa sana ya malezi kutokana na sababu mbalimbali zinazowakumba wazazi wao ikiwemo mazingira ya kazi, wazazi kutengana, shughuli za kilimo, biashara na mtindo wa maisha wa sasa…sasa tusipozingatia malezi stahiki kwa watoto wetu, tutakuwa tunazalisha kizazi cha ajabu katika jamii yetu.” Amesema Kihongosi na kuongeza;

“Ndugu zangu ndiyo maana Serikali yetu inafanya jitihada hizi ili kuwalinda watoto, hivyo sisi kwama wazazi au walezi ni vema tukaunga mkono jitihada za Serikali yetu katika malezi na makuzi bora kwa watoto wa taifa hili.”

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma, Mwanaisham Nassor ambaye kwenye kikao hicho alimuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alisema mtoto ili akue kiafya, kisaikolojia ni lazima tumlee kuanzia mimba inapotungwa.

“Jamii inapaswa kufahamu kuwa malezi ya mtoto yanaanza tangu mimba inapotungwa kwa maana ya umri wa 0 hadi miaka 8, hapo ndipo ubongo wa mtoto unapoundwa, ubongo wake wakati huo ndiyo unapokea vitu vizuri na kukataa vituo vibaya…hivyo ni muhimu kuanza kulea mimba mpaka umri wa miaka 8…kwa kufanya hivyo tutaenda kuleta jamii yenye malezi bora na itatumika baadaye katika nyanja mbalimbali kwa kuwa na wataalam wenye uwezo wa kutoa maamuzi sahihi katika familia zao na kwa taifa kwa ujumla.” Alisema Nassor na kuongeza;

“Matarajio yetu kwa Mji wa Tunduma ni kwamba Mpango huu kufika kwenye kata, mitaa na hata katika ngazi ya familia na vituo ambako watoto wanalelewa, tunayoenda kuyazungumza ni masuala ya lishe, masuala ya elimu na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto…ili kujenga misingi imara ya watoto wetu tangu wanapoingia tumboni kwa mama zao mpaka wanafika miaka 8 hapo tutakuwa tumejenga ubongo mzuri wa mtoto na tutakuwa na jamii ambayo kisaikolojia na kimwili ipo sawa.”

Akizungumza alipokuwa akiwasilisha wasilisho la Sayansi ya MMMAM wakati wa uzinduzi wa Programu hiyo Msimamizi wa Miradi wa Shirika la HIMSO Mkoa wa Songwe na Mbeya, Mwita Isaya amesema kigezo kikubwa ambacho kinawasaidia watoto katika ukuaji wao wa ubongo ni kucheza.

“Michezo kwa watoto ni jambo muhimu sana katika makuzi yao, sasa hapo tukiangalia kwenye jamii yetu siku hizi watoto wengi hawachezi, hata shuleni tu hawachezi, yaani unakuta mtoto wa miaka minne anapambana na daftari kuandika sijui mama, baba, kitu ambacho si sahihi, kwenye michezo kwa umri huo ubongo unakua kwa kiasi kikubwa sana.” Amesema Isaya na kuongeza;

“Ndugu zangu mtoto katika umri huo akikosa kucheza anakuwa amekosa kujifunza vitu vingi ikiwemo, uongozi, uvumilivu, mawasiliano na mambo mengine mengi."

Serikali kwa kushirikiana na Mtandao wa MMMAM Tanzania - TECDEN imedhamiria kuzindua Programu hii kuanzia ngazi ya Taifa hadi ngazi ya Jamii.

Utambulisho wa Programu hiyo katika Mkoa wa Songwe unasimamiwa na Shirika la HIMSO - Health & Insurance Management Services Organisation.

Programu hiyo kwa ngazi ya Taifa ilizinduliwa rasmi Desemba 2021 ambapo kwa Mkoa wa Songwe uzinduzi ulifanyika tarehe 21 Septemba 2023.


Matukio katika Picha:

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi (katikati) akizungumza wakati akizindua rasmi Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), hafla ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024. Kulia ni Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na kulia ni muwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Abubakar Mfaume.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba wakiwa katika hafla fupi ya akizindua rasmi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi.

Msimamizi wa Miradi wa Shirika la HIMSO Mkoa wa Songwe na Mbeya, Mwita Isaya akiwasilisha wasilisho la Sayansi ya MMMAM wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi.

Chifu Msaidizi wa Tunduma, Princewell Siame akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi.

Mwakilishi wa BAKWATA Tunduma, Sheikh Abdillah Mohamed akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi.

Viongozi na Wtalaam mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM), ambayo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 09 Februari 2024. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi.

Pichani ni Afisa Tarafa wa Tunduma, Damson Mwamahonje (katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM), tukio ambalo limefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Tunduma leo tarehe 09 Februari 2024. Kulia ni Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na kulia ni muwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Abubakar Mfaume.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa