• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Madaktari Bingwa Wawasili Songwe

Imewekwa : September 30th, 2024

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, tarehe 30 Septemba 2024 amewapokea Madaktari 36 Bingwa na Bobezi wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan ambao watatoa huduma katika Hospitali zote tano za Halmashauri.

Seneda amewakabidhi kwa Madaktari hao kwa Wakuu wa Wilaya kwa ajili ya kwenda kuanza kazi kwenye Halmashauri zote tano. Madaktari hao watagawanyika katika makundi 5 ambao watakwenda kwenye kila Halmashauri.

Wataalam hao watatoa huduma kwa Wananchi kupitia Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tunduma, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba (Chitete), Hospitali ya Wilaya ya Ileje (Itumba), Hospitali ya Wilaya ya Mbozi (Vwawa) na  Hospitali ya Wilaya ya Songwe.

Kila kundi litakuwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Ukunga, Daktari Bingwa wa Watoto na Wabobezi wa Watoto Wachanga, Daktari Bingwa wa Upasuaji na Bobezi wa Mfumo wa Mkojo, Daktari Bingwa wa Usingizi na Ganzi, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno, Muuguzi Bingwa na Daktari Bingwa wa Mifupa.

"Matibabu  yatatolewa kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa hospitali, wenye kadi zao za bima watatumia kadi, wenye uwezo wa kulipia huduma watalipia na wale ambao italazimika kutibiwa kwa msamaha nao watahudumiwa na hii ni kuhakikisha Wananchi wananufaika na ujio huu wa Madaktari wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan." Amesema Seneda.

Madaktari Bingwa watatoa huduma katika wa Hospitali hizo kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 30 Septemba 2024 hadi tarehe 06 Oktoba 2024 ambapo pia pamoja na mambo mengine watatoa mafunzo elekezi kwa Wataalam wa ndani.

Katibu Tawala huyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha Mkoa huo kutoa huduma za mionzi kwenye vituo 13 ikiwemo huduma za CT - Scan ambazo tayari zimeanza kutolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.

"Tunamshukuru Rais Samia kwa maono yake katika kuboresha Sekta ya Afya, Wananchi tunaendelea kuiunga mkono Serikali katika juhudi zake za kutafuta afya bora kwa wote lakini pia nawapongeza Watumishi wa Sekta hii kwa kazi yenu ngumu ya kuwahudumia Wananchi." Amesema Seneda.

:

Chanzo: @mkoa_wa_songwe

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mei Mosi Songwe Yafana

    May 01, 2025
  • Chaurembo Awapongeza Walimu

    April 30, 2025
  • Tunduma kwa Taaluma Sina Mashaka Nanyi: RAS Seneda

    April 30, 2025
  • Chaurembo Afungua Mafunzo Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili

    April 29, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa