• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Dirisha la Mikopo Lafunguliwa Tunduma

Imewekwa : September 30th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Katibu Tawala wa Wilaya ya Momba, Frank Nkinda amewaasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wakati wa mchakato wa utoaji wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%) kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.

Nkinda ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Usimamizi na Utoaji wa Mikopo kwa makundi hayo kuhusu Kanuni na Mwongozo wa Usimamizi wa Utoaji wa Mikopo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Tunduma na Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo hiyo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 30 Septemba 2024 ambapo amesema Dirisha linafunguliwa rasmi tarehe 01 Oktoba 2024.

"Maafisa Maendeleo niwaombe mtambue kuwa mnapaswa kufuata taratibu zote za utoaji wa mikopo hii kwa uadilifu mkubwa. Ni lazima tuhakikishe kwamba kila kikundi kinachopokea mkopo kina sifa stahiki, na fedha hizi zinawafikia walengwa husika na si vinginevyo," Amesema Nkinda ambaye kwa mujibu wa Mwongozo ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Wilaya ya Uhakiki wa Mikopo.

Katika hatua nyingine, Maafisa Maendeleo ya Jamii wamepewa jukumu la kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.

"Pia, hakikisheni mnatoa elimu kwa Makundi hayo ili wajitokeze kujiandikisha na kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024 kwa wanavikundi wote watakaokuja kuchukua mikopo." Amesisitiza Nkinda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo ameieleza Kamati hiyo kuwa mpaka sasa Halmashauri hiyo inazo shilingi bilioni 4.1 ambazo zinatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya mikopo hiyo ya Asilimia Kumi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti niwataarifu tu Wajumbe kuwa tangu Serikali ilipositisha utoaji wa mikopo hii mwezi Aprili 2023, tuliendelea kufuatilia marejesho kwa vikundi ambavyo tayari vilikuwa na mkopo lakini pia tuliendelea kutenga asilimia kumi (10%) ya fedha za mapato ya ndani, ambapo mpaka sasa dirisha linafunguliwa Halmashauri ya Mji Tunduma inazo shilingi bilioni 4.1, fedha ambazo mpaka kufikia tarehe 30 Oktoba 2024 zinatakiwa kuwa zimeshakopeshwa kwa makundi hayo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Naye Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma, Mwanaishamu Nassor ameeleza kuwa sababu iliyosababisha mikopo ya Asilimia Kumi (10%) kusimama kwa muda ilikuwa ni kufanya maboresho ya kanuni za utoaji mikopo ili mikopo inayotolewa iwe na tija kwa jamii.

"Maboresho yamefanyika katika suala la umri kwa upande wa vijana ambapo kwa sasa umri wa kijana umeongezeka kuanzia miaka 18 hadi miaka 45 wakati awali kigezo kilikuwa ni kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 35 hivyo, marekebisho hayo yameongeza wigo kwa vijana wengi kupata mikopo hii.” Amesema Nassor.

Nassor ameeleza kuwa kigezo kingine kwa wanakikundi kupata mkopo huo ni kuwa na namba ya NIDA kwani uwepo wa namba hiyo utarahisha upatikanaji wa taarifa muhimu za mkopaji katika mfumo.

Ameongeza kuwa ili kuongeza ufanisi zaidi wa utoaji wa mikopo, Divisheni ya Maendeleo ya Jamii itafanya ukaguzi wa andiko la biashara husika, soko pamoja na kuangalia uhalisia wa biashara kabla ya kutoa mikopo kwa wakopaji kwani hii itasaidia kupunguza hasara kwa wanufaika wa mikopo hiyo.

Nassor amesisitiza wakopaji wote wa mikopo ya Asilimia Kumi (10%) watatakiwa kuhakikisha kuwa wanarejesha kwa wakati marejesho yao ili kutoa nafasi ya watu wengine kukopa.

 Mikopo ya Asilimia Kumi (10%) hutolewa kila robo mwaka kwa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu, ili kuwasaidia kujiinua kiuchumi.

Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa