• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

BARAZA LA MADIWA LAPITISHA RASIMU YA SHERIA YA CHAKULA CHA MCHANA MASHULENI

Imewekwa : February 1st, 2022

Na, William Maganga Tunduma

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Mji Tunduma Wilayani Momba Mkoa wa Songwe wamepitisha Rasimu ya sheria ndogo ya uchangiaji wa chakula cha mchana katika shule zote za Serikali ili kupunguza utoro na kuongeza kiwango Cha ufaulu kwa wanafunzi.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Mhe. Ayubu Mlimba alisema wameamua kupitisha sheria hiyo kwa shule zote za Serikali za kutwa  wakiwa na lengo la kuwasaidia watoto wadogo kuanzia shule za awali mpaka Sekondari.



Alisema mkakati wa kutunga sheria ndogo hizo umezingatia matakwa ya sheria ya Bunge Kwa Tangazo la Halmashauri la Agosti 10, 2021 la nia ya kutunga sheria ndogo.


*”Sheria ndogo hii imejadiliwa na kamati za maendeleo ya kata kwa mujibu wa kifungu namba 81(1) Cha sheria ya Serikali za mitaa”* alisema Mlimba.


Alisema mchakato huo wa sheria utakapo pita baada ya kupelekwa ngazi ya Mkoa na hatimaye Bungeni utakapo rudi unawataka wazazi na walezi wa wanafunzi kuchangia debe mbili za mahindi na kilo kumi za maharage kwa kila mwaka ili kuwasaidia watoto wao wakiwa shuleni.


Mkurugenzi wa Mji Tunduma Philmon Magesa alisema sheria hiyo itasaidia  kwa kiasi kikubwa ongezeko wazazi na walezi kuchangia watoto wakiwa shuleni tofauti na ilivyo hivi sasa.


*”Suala la utoaji chakula kwa shule za Mji Tunduma mpaka hivi sasa linaenda kwa kusuasua ni asilimia 50 tu chakula hutolewa, suala la uchangiaji limekuwa likitumiwa kwa hiyali sasa tumeamua kutumia kifungu kinachotupa nguvu ya kutunga sheria, Ambapo hivi sasa uchangiaji chakula kwa shule zote za Serikali kuanzia awali mpaka Sekondari ni lazma na sio hiyari tena"* alisema Magesa.



Alisema umuhimu na sababu za kutunga sheria ndogo kuwa ni kuweka utaratibu wa uchangiaji wa chakula mashuleni unaizingatia utaratibu wa kisheria, kuwatia watoto motisha na kupunguza utoro mashuleni, kuongeza mahudhurio na ufaulu hasa mitihani ya Taifa pamoja na kuwarahisishia watekelezaji wa mpango wa uchangiaji chakula kusimamia utekelezaji kupitia utaratibu uliopo kisheria.


Mbunge Viti maalum mkoa wa Songwe Mhe. Neema Mwandabila alisema uchangiaji chakula mashuleni utekelezaji wake awali ulikuwa mgumu, huku akidai kuwa sheria hiyo walioipitisha Madiwani kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka uchangiaji na ufaulu kuongezeka.




Alisema Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa udumavu hivyo watoto kupata chakula shuleni kutasaidia watoto kuhimili masomo kwa muda mrefu.


Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Tunduma Adv. Timotheo Massawa alisema kupitia kifungu Cha saba (7) kinaeleza kuwa *mzazi au mlezi atakuwa ametenda kosa iwapo atashindwa au kukataa kwa makusudi kumchangia mtoto gharama za chakula Cha mchana*


"Kwa kupitia kifungu namba kumi (10) kinampa mamlaka mkurugenzi kutoza faini isiyozidi shilingi 50,000 kwa mtu yeyote iwapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa faini iliyoainishwa chini ya sheria ndogo hii" alisema Massawa.




Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mei Mosi Songwe Yafana

    May 01, 2025
  • Chaurembo Awapongeza Walimu

    April 30, 2025
  • Tunduma kwa Taaluma Sina Mashaka Nanyi: RAS Seneda

    April 30, 2025
  • Chaurembo Afungua Mafunzo Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili

    April 29, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa