Mkurugenzi wa mji wa Tunduma Bi. Regina Bieda akigawa mabati Bandle 262 yaliyo gharimu pesa za kitanzania 78,047,732.15 ambayo yanakwenda kupaua vyumba 63 vya madarasa ndani ya Mji wa Tunduma
Mkurugenzi wa Tunduma Bi. Regina Bieda kulia akiongea na watumishi wa
Idara ya elimu Sekondari na Msingi wakati wa kuwakabidhi Mabati
Bi. Regina amesema “Nawataka wote mkasimamie upauaji wa maboma yote kwani Mabati haya tumeamua kununua kiwandani hasa kwa lengo la kupata Bidhaa bora na zenye viwango huku tukiokoa fedha za Serikali”
Pia Mkurugenzi aliwashukuru wafanyakazi wa Halmashauri ya mji wa Tunduma kwa kushikamana katika kukusanya mapato kwani pesa za kununulia mabati hayo ni za mapato ya ndani.
“Pesa hizi ni za walipakodi hivyo tunatakiwa kuhakikisha hakuna kununua vitu ambavyo havina ubora ndomaana tumeamua kuchukua mabati yenye ubora na uimara moja kwa moja toka kiwandani tukiwa na uhakika nayo sio ya kununua mitaani”
Pia ameeleza “tutaendelea kununua vifaa vya Idara ya Elimu mara tunapopata bajeti. Tutaendelea kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuhakikisha miradi ya maendeleo kwa ujumla inasonga mbele”
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957389
Simu ya Mkononi: +255 754 549 511
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa