Mkurugenzi wa Halmashauriya Mji wa Tunduma, Kastori Msigala, amewahimiza watumishi wa Halmashauri hiyokuendelea kuchapa kazi baada ya kupokea hati inayoridhisha iliyotokana nataarifa ya ukaguzi uliofanywa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali (CAG).
Mkurugenzi alitoakauli hiyo leo hii alipoongea na wafanyakazi wa Halmashauri yake baada yakupokea ripoti ya CAG iliyobainisha kwamba Halmashauri ya Mji wa Tunduma nimiongoni mwa Halmashauri nchini zilizopata hati inayoridhisha.
“Tunatakiwa kufanyakazi kwa weledi na ari zaidi ili tuendelee kupata hati safi,” alisema Bw.Msigala, na kuongeza kwamba hati hii ni tija kwa wafanyakazi pamoja na wananchiwa Tunduma kwani inadhihirisha pesa zinazokusanywa zinatumika vema.
Mkurugenzi ameendeleakusisitiza kwamba atahakikisha anaendelea kusimamia matumizi mazuri ya fedha zaSerikali, kwani ndiyo njia sahihi ya kuhakikisha kwamba fedha za mlipa kodizinatumika kwa ajili ya shughuli za maendeleo, na si kutumika bila kuwa namaelezo sahihi.
“Nitaendelea na msimamowangu wa kutopitisha malipo yoyote kama hayajakaguliwa na Mkaguzi wa Ndani waHesabu za Serikali wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma,” amesisitiza Bw. Msigala.
Halmashauri ya Mjiwa Tunduma imepata hati inayoridhisha baada ya taarifa ya ukaguzi wa hesabuzake za mwaka wa fedha 2016/2017 iliyokabidhiwa kwa Rais Dkt John PombeMagufuli mwishoni mwa mwezi wa tatu, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hati hiyo imetolewabaada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Asaadkuridhika na hesabu za mapato na matumizi ya miradi mbalimbali ya Halmashaurihiyo.
Kupata Ripori hiyo bonyeza hapa LOCAL-GOVERNMENT-AUTHORITIES-GENERAL-REPORT_2.pdf
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957389
Simu ya Mkononi: +255 754 549 511
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa