Waziri Mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela kuhakikisha eneo la wazi la mpaka wa Tanzania na Zambia unaendelea kubaki wazi ili kukomesha magendo na rushwa mpakani hapo.
Akizungumza na wananchi Wa Tunduma, 6 Julai 2020 Majaliwa amesema kitendo cha mpaka huo kusongwa na shughuli nyingine ikiwemo makazi, kinachangia kuwepo biashara za magendo na rushwa na kufanya halmashauri kushindwa kukusanya mapato ambayo yanawezesha kuweka miradi ya maendeleo.
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957389
Simu ya Mkononi: +255 754 549 511
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa